Huawei watangaza rasmi kuja na mfumo endeshi (OS) wao mpya kwa ajili ya simu zao na kompyuta mpakato mwanzoni mwa mwaka 2020. Mkurugenzi mtendaji wa Huawei upande wa Consumer Business Group, Richard Yu, alisema mfumo endeshi wao mpya upo tayari kwa ajili ya simu na kompyuta, na utaanza kutumika katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka huu (Q4) nchini China, ila kuanzia robo ya kwanza (Q1) na ya pili (Q2) ya mwaka 2020 ndipo utaachiwa kutumika rasmi kwa nchi zingine nje ya China. Mfumo endeshi huo utakuja na soko la app zake linaloitwa App Gallery mkabala kushindana na Google Playstore, Yu pia alisema kama Huawei watazuiwa kabisa kutumia mifumo endeshi kutoka Microsoft na Google basi hawatakuwa na njia nyingine zaidi ya kutumia mfumo endeshi wao huo mpya. Google walitangaza kusitisha huduma ya Android kwa Huawei, baada ya kampuni hiyo kuwekwa kwenye orodha ya 'Entity List' na serikali ya Marekani - Hii inamaana kampuni yoyote nchini Marekani ikitaka kufanya biashara na Huawei lazima ipate kibali kutoka serikalini. #andrewsoft #teknolojia #simu

Uamuzi wa Mbunge huyo wa Segerea umetangazwa leo Mei 16,2019 Bungeni jijini Dodoma kupitia Spika wa Bunge, Job Ndugai ambapo amesema ameeleza kupata taarifa kutoka kwa mbunge huyo.
“Nimetaarifiwa kuwa Mheshimiwa Bonnah amebadili jina na sasa anatumia jina la Bonnah Ladislaus Kamoli”, amesema Spika Ndugai.
April 28, 2019 kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mbunge huyo wa Segerea aliandika ujumbe kwamba tuhuma ambazo zilikuwa zikisambaa kwenye mtandao wa kijamii kuwa alifumaniwa na mumewe hazikuwa na ukweli.
"Wahenga wanasema jambo likiongelewa sana bila majibu linaweza kugeuka likawa kweli. Sasa ni hivi mimi Bonnah Ladislaus Kamoli au jina langu lingine Neema, sijawahi kufumaniwa hata siku moja katika maisha yangu". aliandika Bonnah
"Sio kwamba mimi ni muadilifu sana au malaika ila hapakuwepo na mtu wa kunifumania nadhani mtakua mmenielewa na sitaongea tena na kama kuna mtu ana ushahidi alete na kanifumania na nani", alimaliza Bonnah katika maelezo yake.
Reference From EATV.