Sunday, May 12, 2019

BREAKINGNEWS MANCHESTER CITY BINGWA EPL 2018/19

Timu ya Manchester City imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini England #EPL kwa mara ya pili mfululizo baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wake wa mwisho uliomalizika hivi punde na kuhitimisha msimu ikiwa kileleni.

Man City wakiwa ugenini wameichapa Brighton & Hove Albion mabao 4-1 na kufikisha pointi 98 juu ya wapinzani wao wa karibu Liverpool ambao nao wameshinda 2-0 dhidi ya Wolves na kumaliza msimu wakiwa nafasi ya pili na pointi 97.

Neno moja la pongezi kwao, huku ukitoa maoni yako unadhani nini kinawaangusha Liverpool kwenye #EPL?

No comments:

Post a Comment