Followers

Saturday, May 25, 2019

Huawei Kutangaza Vita na Kampuni ya IPhone kwa Kutoa simu Kali cheki.

Huawei watangaza rasmi kuja na mfumo endeshi (OS) wao mpya kwa ajili ya simu zao na kompyuta mpakato mwanzoni mwa mwaka 2020. Mkurugenzi mtendaji wa Huawei upande wa Consumer Business Group, Richard Yu, alisema mfumo endeshi wao mpya upo tayari kwa ajili ya simu na kompyuta, na utaanza kutumika katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka huu (Q4) nchini China, ila kuanzia robo ya kwanza (Q1) na ya pili (Q2) ya mwaka 2020 ndipo utaachiwa kutumika rasmi kwa nchi zingine nje ya China. Mfumo endeshi huo utakuja na soko la app zake linaloitwa App Gallery mkabala kushindana na Google Playstore, Yu pia alisema kama Huawei watazuiwa kabisa kutumia mifumo endeshi kutoka Microsoft na Google basi hawatakuwa na njia nyingine zaidi ya kutumia mfumo endeshi wao huo mpya. Google walitangaza kusitisha huduma ya Android kwa Huawei, baada ya kampuni hiyo kuwekwa kwenye orodha ya 'Entity List' na serikali ya Marekani - Hii inamaana kampuni yoyote nchini Marekani ikitaka kufanya biashara na Huawei lazima ipate kibali kutoka serikalini. #andrewsoft #teknolojia #simu

Wednesday, May 22, 2019

Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 23.05.2019

Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 23.05.2019: Terry, Cancelo, Trippier, Rakitic, Wan-B Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 23.05.2019: Terry, Cancelo, Trippier, Rakitic, Wan-Bissaka

Saa 2 zilizopita

Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii WhatsApp Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Twitter Mshirikishe mwenzako David milanzi


John TerryHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJohn Terry

Nahodha wa zamani wa England na Chelsea John Terry, ambaye kwa sasa ni naibu meneja wa Aston Villa, anashauriana na Middlesbrough kuhusu uwezekano wa kuwa maneja wao mpya.(Talksport)
Manchester City wanakaribia kumsajili beki wa Ureno Joao Cancelo, 24, ambaye thamani yake inakadiriwa na Juventus kuwa euro milioni 60. (Record - in Portuguese)
Atletico Madrid na Napoli wanapania kumsajili beki wa kulia wa Tottenham na mchezaji wa kimataifa wa England Kieran Tripper, 28. (Mirror)

Tarehe 7 Septemba 2019: Siku aliyotangaza Tundu Lissu kurudi nyumbani Tanzania.

Tarehe 7 Septemba 2019: Siku aliyotangaza Tundu Lissu kurudi nyumbani Tanzania.


Mbunge wa Singida Mashariki kupitia chama cha Chadema na mnadhimu mkuu wa upinzani Tanzania Tundu Lissu ametangaza kwamba atarudi nchini humo tarehe saba mwezi wa tisa ikiwa ni miaka miwili tangu aliposhambuliwa.
Akizungumza kwa njia ya simu na kupitia runinga ya Chadema mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe katika makao makuu ya Chadema Lisu amesema kuwa atarudi nchini Tanzania siku hiyo ili kuadhimisha kushambuliwa kwake.
''Nitatua tarehe saba mwezi septemba 2019 kwenye ardhi ya tanzania kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nitakuwepo, alisema Tundu Lissu

Thursday, May 16, 2019

Mbunge aliyetuhumiwa kufumaniwa,....

Mbunge aliyetuhumiwa kufumaniwa abadilisha jina

ALHAMISI , 16TH MEI , 2019
Mbunge wa Segerea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bonnah Kaluwa ametoa taarifa ya kubadilisha jina kufuatia kuingia kwenye mvutano wa matumizi ya jina na mume wake Moses Kaluwa ambapo sasa atafahamika kwa jina la Bonnah Kimoli.
Uamuzi wa Mbunge huyo wa Segerea umetangazwa leo Mei 16,2019 Bungeni jijini Dodoma kupitia Spika wa Bunge, Job Ndugai ambapo amesema ameeleza kupata taarifa kutoka kwa mbunge huyo.
Nimetaarifiwa kuwa Mheshimiwa Bonnah amebadili jina na sasa anatumia jina la Bonnah Ladislaus Kamoli”, amesema Spika Ndugai.
April 28, 2019 kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mbunge huyo wa Segerea  aliandika ujumbe kwamba tuhuma ambazo zilikuwa zikisambaa kwenye mtandao wa kijamii kuwa alifumaniwa na mumewe hazikuwa na ukweli.
"Wahenga wanasema jambo likiongelewa sana bila majibu linaweza kugeuka likawa kweli. Sasa ni hivi mimi Bonnah Ladislaus Kamoli au jina langu lingine Neema, sijawahi kufumaniwa hata siku moja katika maisha yangu". aliandika Bonnah
"Sio kwamba mimi ni muadilifu sana au malaika ila hapakuwepo na mtu wa kunifumania nadhani mtakua mmenielewa na sitaongea tena na kama kuna mtu ana ushahidi alete na kanifumania na nani", alimaliza Bonnah katika maelezo yake.
Reference From EATV.

Tuesday, May 14, 2019

Bunge la A.Mashaliki Kupinga Vipodozi vinavyo Badili langi ya Mwili.

Bunge la Afrika Mashariki (EALA) limepitisha azimio linalotoa wito wa kuwekwa kwa marufuku dhidi ya watengenezaji na waagizaji wa bidhaa zenye kemikali ya hydroquinone.

Bidhaa hizo ni pamoja na sabuni, mafuta na urembo wenye kemikali ya hydroquinone inayobadilisha ngozi kuwa nyeupe.

Hydroquinone ni kemikali inayopatikana katika aina mbali mbali za bidhaa mbali mbali za mwili ambayo kwa kawaida imetengenezwa kwa ajili ya kuifanya ngozi kuwa nyeupe.

Serikali yatowa hatima kuhusu kuonyesha chaneli za Ndani, Ving'amuzi vyote Nchini.

Serikali yatoa maamuzi kuhusu ving'amuzi kuonesha

JUMANNE , 14TH MEI , 2019
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Atashasta Nditiye, amesema serikali inashughulikia maombi ya makampuni yanayotaka leseni ya kubeba maudhui ya vituo vya televisheni vya ndani ili yaweze kupata leseni stahiki.
Satelite
Naibu Waziri huyo ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Nyamagana kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe. Stanslaus Mabula, aliyetaka kujua kama serikali haioni kufungia ving'amuzi vya Azam TV, DSTV na vinginevyo kuonesha vituo vya televisheni vya hapa nchini kuonekana katika vingamuzi hivyo ni kuwanyima raia haki ya kupata  taarifa.
Mhe. Nditiye amesema serikali inatambua umuhimu wa wananchi kupata fursa ya kujua mambo  yanayoendelea kwenye taifa, kwa misingi hiyo imetoa leseni zenye masharti tofauti ikiwemo leseni za utangazaji wa umma ambapo matangazo huruhusiwa kurushwa na watoa huduma wote.
Amesema kwa sasa matangazo ya umma ni TBC 1 na TBC 3 maarufu kama Safari Channels na kuongeza kuwa makampuni yanayomiliki visimbuzi vya  DSTV, ZUKU na AZAM TV, hayakustahili kutoa huduma ya  kubeba vituo vya televisheni vya hapa nchini kutokana na masharti ya leseni zao.

Sunday, May 12, 2019

BREAKINGNEWS MANCHESTER CITY BINGWA EPL 2018/19

Timu ya Manchester City imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini England #EPL kwa mara ya pili mfululizo baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wake wa mwisho uliomalizika hivi punde na kuhitimisha msimu ikiwa kileleni.

Man City wakiwa ugenini wameichapa Brighton & Hove Albion mabao 4-1 na kufikisha pointi 98 juu ya wapinzani wao wa karibu Liverpool ambao nao wameshinda 2-0 dhidi ya Wolves na kumaliza msimu wakiwa nafasi ya pili na pointi 97.

Neno moja la pongezi kwao, huku ukitoa maoni yako unadhani nini kinawaangusha Liverpool kwenye #EPL?

Friday, May 10, 2019

MUGABE KUFILISIKA

MUGABE  KUFILISIKA
..!?

Zana za kilimo za rais wa zamani wa Zimbabwe zinapigwa mnada hapo kesho  tarehe 11 /05 kutokana na deni linalomkabili kiongozi huyo alieondolewa madarakani. Zana hizo zipo shambani kwake.

SERIKALI KUONGEZA NDEGE NYINGINE



Ili kuboresha utendaji wa Shirika la ndege Tanzania (ATCL) kwa mwaka wa fedha 2019/2020 serikali imetenga fedha kwa ajili ya kukamilisha malipo ya Ndege ya Pili aina ya Boeing 787 Dreamliner na ndege ya nne aina ya Bombadier Q400

Pia itafanya malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mbili mpya aina ya A220-300

Ununuzi wa ndege moja aina ya Bombadier Q400 na injini ya akiba kwa ajili ya ndege aina ya Bombadier Q400


Thursday, May 9, 2019

MECHI ZOTE ZA LIGIKUU TANZANIA BARA HIZI HAPA.

Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Ijumaa.

Je Simba SC watalipa kisasi cha kufungwa na Kagera Sugar katika mechi ya kwanza ama Kagera Sugar wataendeleza rekodi ya kuchukua point kwa mnyama?

UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WATIKISA.

Muonekano wa sasa wa jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JNIA.

Jengo hilo limesanifiwa kwa viwango vya kimataifa vya daraja 'C' vya Usafiri wa Anga (IATA) na linatarajiwa kuwa kituo kikuu cha usafiri wa anga na kuleta tija kwa Tanzania.

Weka komenti yako hapo chini.



Wednesday, May 8, 2019

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini Usharika wa Moshi Mjini.

Hapa ni Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini Usharika wa Moshi Mjini, sehemu ambapo itafanyika ibada ya mwisho ya kuaga mwili wa Dr. Mengi kesho Mei 9, 2019.

#RIPDrMengi



Alichokisema Askofu Josephtat Gwajima.

Askofu Josephat Gwajima adai mkanda wa picha za ngono umetangenezwa na maadui zake.
Polisi wanaendelea na uchunguzi kujuwa ukweli wa mambo. Sema neno moja tu.

Kwalichofanya Wakina Mama Uko Mkoani Hai.

Wakina mama wanasema gari lililobeba mwili wa mpendwa wetu Dr. Reginald Mengi likipita katika khanga na vitenge vyao, itakuwa ni baraka kwao kwa yale mema aliyoyatenda.

#RIPDrMengi

Mkuu wa wilaya ya Hai

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, ni miongoni mwa waombolezaji waliofika hapa kati
ka Uwanja wa Ndege wa KIA, tayari kuupokea mwili wa mpendwa wetu Dr. Mengi.

#RIPDrMengi

Makonda amchana Mbowe Corona aina Uchama.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewaomba viongozi wa vyama vya siasa nchini, kuungana kwa pamoja katika kipindi h...