Tuesday, May 14, 2019

Bunge la A.Mashaliki Kupinga Vipodozi vinavyo Badili langi ya Mwili.

Bunge la Afrika Mashariki (EALA) limepitisha azimio linalotoa wito wa kuwekwa kwa marufuku dhidi ya watengenezaji na waagizaji wa bidhaa zenye kemikali ya hydroquinone.

Bidhaa hizo ni pamoja na sabuni, mafuta na urembo wenye kemikali ya hydroquinone inayobadilisha ngozi kuwa nyeupe.

Hydroquinone ni kemikali inayopatikana katika aina mbali mbali za bidhaa mbali mbali za mwili ambayo kwa kawaida imetengenezwa kwa ajili ya kuifanya ngozi kuwa nyeupe.

No comments:

Post a Comment