Followers

Monday, October 21, 2019

Honyo Kwa Vyama Vya Siasa,Hatuwakali kuchukuliwa kwa Atakae Kiuka.

Vyama vya siasa vyaonywa, hatua kali kuchukuliwa

JUMATATU , 21ST OCT , 2019
Serikali wilayani Kilombero mkoani Morogoro imevionya baadhi ya vyama vya siasa, kuacha mara moja kutoa vitisho kwa wanachama na viongozi, ambao wamehama na kujiuzulu kwenye vyama vyao, kufuatia kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanachama wakidai kuwa wanapokea taarifa za vitisho.
Nembo za vyama mbalimbali vya siasa
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo, wakati wa mkutano na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapo, kwa ajili kujadili changamoto zinazowakabili, ambapo amesema kuwa amepokea taarifa za baadhi ya wanachama ambao wamehama vyama vyao kutishiwa usalama wao.
Kwa upande wake aliyekuwa Diwani wa kata ya Katindiuka kupitia CHADEMA, Furaha Mganya, amesema kuwa amesikitishwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimfuatilia na kutaka kujua kwanini amejiuzulu nafasi yake na kuhamia CCM.
Kwenye mkutano huo Mbunge wa viti maalumu kupitia (CCM) Dkt Gertrude Rwakatare, amegawa baiskeli 300 zenye thamani ya shilingi milioni 45, kwa watendaji wa CCM wilayani Kilombero ili kuwarahisishia watendaji hao utakelezaji wa majukumu yao, huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, Novemba 24 mwaka huu.


Tuesday, October 15, 2019

Matokeo ya darasa la saba 2019 haya hapa


     Matokeo ya         darasa la saba       2019 haya hapa
TUESDAY OCTOBER 15 2019


Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde 
By David Assa Milanzi
Milanzidavid92@gmail.com
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 ambapo asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369 wamefaulu mtihani huo huku watahiniwa 909 wakifutiwa matokeo kwa sababu ya udanganyifu.
Akitangaza matokeo hayo  leo Jumanne Oktoba 15, 2019 Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde amesema kwa jumla yanaonyesha ufaulu umeongezeka kwa asililia 3.78 lakini ufaulu katika somo la Kiingereza bado ni mdogo likilinganishwa na masomo mengine.
"Ufaulu katika somo la Kiingereza unaendelea kuimarika mwaka hadi mwaka hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kuendelea kufanyika ili kuinua kiwango cha ufaulu katika somo hili," amesema Dk Msonde.
Aidha katika matokeo hayo, Grace Imori Manga wa shule ya msingi Graiyaki ya mkoani Mara ametangazwa kuwa wa kwanza kitaifa akifuatiwa na Francis Gwani wa shule ya msingi Paradise ya mkoani Geita na namba tatu imeshikiliwa na Loi Kitundu wa Shule ya msingi Mbezi ya Dar es Salaam.
Wengine katika orodha ya 10 bora ni Victor Godfrey wa shule ya msingi Graiyaki, Azizi Yassin wa Graiyaki goldie Hhayuma wa Graiyaki, Daniel Daniel wa shule ya msingi Little Mkoani Shinyanga, Hilary Nassor wa Peaceland ya Mwanza, Mbelele Mbelele wa Kwema Modern ya Shinyanga na Nyanswi Richard wa Graiyaki ya Mara.
Shule 10 bora kitaifa ni Graiyaki ya Mara, Twibhoki ya Mara, Kemebos ya Kagera, Little Treasures ya Shinyanga, Musabe ya Mwanza, Tulele ya Mwanza, Kwema Morden ya Shinyanga, Peaceland ya Mwanza, Mugini ya Mwanza na Rocken Hill ya Shinyanga.
Kimkoa, Mkoa wa Dar es Salaam umeshika namba moja ukifuatiwa na Arusha, Iringa, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Mbeya, Simiyu, Njombe na Pwani.
Halmashauri 10 bora zimeongozwa na Arusha jiji, Ilemela, Kinondoni, Mwanza jiji, Ilala Manispaa, Moshi Manispaa, Bukoba Manispaa, Iringa Manispaa, Biharamulo na Arusha



Mwananchi

Fusla Mpya 2019 za Ajila Kwa Vijana Wanaopenda Uwigizaji Tanzania.

Full Data hapo chini.
 Vigezo vipo hapo chini.

Monday, October 14, 2019

Kimewaka Uchaguzi wa Serikali ya Mtaa Mzingani - Tanga.

Malalamiko ya Bahadi ya wagombea tulio hojiana nao.
Katika kata ya mzingani tanga mjini katika uchaguzi wa uenyekiti wa serikali ya mtaa.wagombea tumechukua form na tumerudisha zimejadiliwa tawi na mapendekezo yamepekekwa kata hapo kata diwani amebadilisha maksi na mapendezo ya tawi na kuweka ya kwake ili awapitishe watu wake ambao Tunawaifazi Kwa majina na Leo baada ya kubadilisha maksi ameamrisha wapeleke wilaya kwa maana huyo diwani anakiuka katiba ya chama na kuvuruga chama na kugawa watu.


Tunaomba uongozi wa juu mfuatilie hili pia jana katika kikao cha kata amekuna mkurugenzi na kumfokea Katibu na kumwambia mgombea  asiwekewe mwenzake akatwe cha ajabu mkurugenzi inakuaje anakuja katika kikao cha chama na kumpa maagizo kwa kumlazimisha Katibu wa kata kua ahakikishe kampira anapita

Huyu diwani kwa mini analazimisha kwamba watu wake wapitishwe inamaana gani kutuletea form na inamaana gani kuweka makatibu wa matawi kama max na mapendekezo diwani anayafuta na kuandika yakwake
https://www.facebook.com/223171508350475/posts/394219847912306/?app=fbl

Tuwekee Commenti yako hapo chini. 

Makonda amchana Mbowe Corona aina Uchama.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewaomba viongozi wa vyama vya siasa nchini, kuungana kwa pamoja katika kipindi h...