Walinzi wa rais Uhuru Kenyatta wamempiga risasi na kumjeruhi mtu aliyejaribu kukwea uzio wa ikulu ya rais jijini Nairobi Kenya.
Kibet Bera ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa 5 wa uhandisi wa mitambo katika chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Jomo Kenyatta(JKUAT) alipigwa risasi begani na hatimaye kukamatwa baada ya kukaidi amri ya walinzi wa ikulu.
Afisa mkuu wa polisi katika kaunti ndogo ya Kilimani, Michael Muchiri amethibitisha kisa hicho kilichotokea siku moja baada ya Bera kuandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa angeshambulia ikulu kutekeleza agizo aliopewa na 'mungu'.
No comments:
Post a Comment