Followers

Tuesday, October 15, 2019

Matokeo ya darasa la saba 2019 haya hapa


     Matokeo ya         darasa la saba       2019 haya hapa
TUESDAY OCTOBER 15 2019


Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde 
By David Assa Milanzi
Milanzidavid92@gmail.com
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 ambapo asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369 wamefaulu mtihani huo huku watahiniwa 909 wakifutiwa matokeo kwa sababu ya udanganyifu.
Akitangaza matokeo hayo  leo Jumanne Oktoba 15, 2019 Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde amesema kwa jumla yanaonyesha ufaulu umeongezeka kwa asililia 3.78 lakini ufaulu katika somo la Kiingereza bado ni mdogo likilinganishwa na masomo mengine.
"Ufaulu katika somo la Kiingereza unaendelea kuimarika mwaka hadi mwaka hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kuendelea kufanyika ili kuinua kiwango cha ufaulu katika somo hili," amesema Dk Msonde.
Aidha katika matokeo hayo, Grace Imori Manga wa shule ya msingi Graiyaki ya mkoani Mara ametangazwa kuwa wa kwanza kitaifa akifuatiwa na Francis Gwani wa shule ya msingi Paradise ya mkoani Geita na namba tatu imeshikiliwa na Loi Kitundu wa Shule ya msingi Mbezi ya Dar es Salaam.
Wengine katika orodha ya 10 bora ni Victor Godfrey wa shule ya msingi Graiyaki, Azizi Yassin wa Graiyaki goldie Hhayuma wa Graiyaki, Daniel Daniel wa shule ya msingi Little Mkoani Shinyanga, Hilary Nassor wa Peaceland ya Mwanza, Mbelele Mbelele wa Kwema Modern ya Shinyanga na Nyanswi Richard wa Graiyaki ya Mara.
Shule 10 bora kitaifa ni Graiyaki ya Mara, Twibhoki ya Mara, Kemebos ya Kagera, Little Treasures ya Shinyanga, Musabe ya Mwanza, Tulele ya Mwanza, Kwema Morden ya Shinyanga, Peaceland ya Mwanza, Mugini ya Mwanza na Rocken Hill ya Shinyanga.
Kimkoa, Mkoa wa Dar es Salaam umeshika namba moja ukifuatiwa na Arusha, Iringa, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Mbeya, Simiyu, Njombe na Pwani.
Halmashauri 10 bora zimeongozwa na Arusha jiji, Ilemela, Kinondoni, Mwanza jiji, Ilala Manispaa, Moshi Manispaa, Bukoba Manispaa, Iringa Manispaa, Biharamulo na Arusha



Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Makonda amchana Mbowe Corona aina Uchama.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewaomba viongozi wa vyama vya siasa nchini, kuungana kwa pamoja katika kipindi h...